• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukaribisha siku za baadeye kwa hatua ya kutekeleza mageuzi

    (GMT+08:00) 2019-01-03 16:39:37

    Mwaka 2019 umewadia. Kati ya habari kumi za kimataifa za mwaka 2018 zilizochaguliwa na vyombo vikubwa vya habari, moja ni ile inayohusu kupamba moto kwa mgogoro wa biashara duniani ambao ulizushwa na Marekani.

    Rais Xi Jinping wa China akikumbusha kuhusu mwaka uliopita kwenye salamu zake za mwaka mpya, alisisitiza kuwa imani na nia ya China katika kulinda mamlaka na usalama wa nchi hazitabadilika, udhati na wema wa China katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja hautabadilika. Hali ambayo imeonesha kuwa, China si kama tu inasukuma mbele mageuzi mbalimbali kwa mujibu wa maagizo yaliyowekwa kwenye Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, ikiwa nchi kubwa inayowajibika, udhati na wema wake wa kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo ya pamoja hautabadilika.

    Kuhimiza maendeleo ya pamoja kunaonesha kuwa China haina wazo la kushindana la kutiana hasara kama nchi nyingine zinavyokuwa nalo katika mchakato wa mafungamano ya kiuchumi duniani. Mwaka 2018 China ilitekeleza hatua mfululizo za mageuzi na ufunguaji mlango, mwelekeo huo utazidi kuimarishwa mwaka huu.

    Kutokana na mtizamo wa dunia, kujilinda kibiashara, na utaratibu wa upande mmoja umekuwa ukifufuka katika miaka ya hivi karibuni kwenye baadhi ya nchi haswa mwaka 2018, biashara huria na mafungamano ya kiuchumi yanakabiliwa na changamoto kubwa. Mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani umepungua baada ya mapambano makali, na pande zote mbili zimekubaliana kutatua ufuatiliaji wao kwa njia ya mazungumzo. Hatua za China za kupanua ufunguaji mlango katika mwaka uliopita na siku zijazo, si kama tu zitasaidia mazungumzo kati ya pande hizo mbili, bali pia zitasaidia maendeleo ya pamoja na nchi mbalimbali.

    Kutokana na kukabiliwa na hali isiyotarajiwa ya uchumi wa dunia na uhusiano wa kimataifa ya mwaka 2019, watu wengi watazingatia zaidi nchi kubwa China na Marekani. Rais Donald Trump wa Marekani pia ametambua kuwa uhusiano kati ya Marekani na China ni muhimu sana ambao unafuatiliwa sana na dunia nzima. Imefahamika kuwa ujumbe wa China na Marekani utafanya mazungumzo ya ana kwa ana mwezi huu. Ingawa matokeo hayajulikani yatakuwaje, lakini kama pande hizo mbili zitafikia makubaliano, hakika yatanufaisha pande zote mbili, na pia kulingana na matarajio ya masoko ya nchi hizo mbili, na kusaidia kulinda utulivu wa uhusiano kati ya China na Marekani na kuchangia dunia nzima.

    Kwa China yenyewe, bila ya kujali matokeo yatakuwaje, ni muhimu zaidi kushughulikia vizuri mambo yake yenyewe, na kuimarisha mageuzi kwa pande zote, ambayo itakuwa hatua thabiti zaidi ya China kwa mwaka 2019 na katika muda mrefu zaidi ujao, vilevile ni ishara imara kwa dunia.

    Mwaka 2018, dunia nzima imeshuhudia kupamba moto kwa mgogoro wa biashara duniani, vilevile imejionea mwendo kasi wa hatua ya mageuzi na ufunguaji mlango wa China. Katika mwaka mpya, dunia vilevile itaona China haitasita katika hatua yake ya kujiendeleza na kupata maendeleo kwa pamoja na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako