• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha anga za juu cha China chatua upande wa mbali wa mwezini

    (GMT+08:00) 2019-01-03 17:11:57

    Chombo cha uchunguzi cha anga za juu cha China kinachojulikana kwa jina la Chang'e-4 kimetua upande wa mwezi na kuwa chombo cha anga cha kwanza kutua eneo hilo ambalo halijawahi kuonekana duniani.

    Kwa mujibu wa idara ya anga za juu ya China (CNSA), chombo hicho kilitua majira ya saa nne na dakika 26 asubuhi kwa saa za Beijing.

    Kwa msaada wa satelaiti ya Queqiao, chombo hicho cha uchunguzi kimefanikiwa kurudisha picha ya kwanza ya karibu ya upande wa mwezi na kufungua ukurasa mpya katika uchunguzi wa mwezi.

    Habari zinaeleza kuwa, wakati wa kutua kwa chombo hicho, kamera maalumu iliyofungwa kwenye chombo hicho cha uchunguzi ilipata picha za eneo ikitua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako