• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mauzo ya Afrika mashariki kwenye soko la Marekani yaongezeka

  (GMT+08:00) 2019-01-03 19:45:08

  Mauzo ya bidhaa za Afrika Mashariki kwenda Marekani yalifikia dola bilioni 1 kati ya Oktoba 2017 na Septemba 2018 hilo likiwa ni ongezeko la asilimia 17 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka 2017.

  Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa limesema bidhaa za nguo ndio ziliuzwa kwa wingi zikichukua asilimia 84.

  Taasisi ya fursa za biashara kwa Afrika Agoa, ambako nchi za kusini mwa jangwa la sahara hupata nafasi ya kuuza zaidi ya bidhaa 6,000 imesaidia kuendelea kuongezeka kwa mauzo hayo.

  Kulingana na taakwimu, Kenya imesalia kuwa muuzaji mkuu wa bidhaa chini ya Agoa ikiwa imeuza bidhaa za dhamani ya dola milioni 454 katika kipindi hicho, Tanzania dola milioni 42, Uganda dola milioni 3 nayo Rwanda ikiuza dola milioni 5.8.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako