• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya rais Xi kuhusu suala la Taiwan ni mwongozo mpya kwa amani, muungano na maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2019-01-04 09:53:31

    Hivi karibuni rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba muhimu kuhusu uhusiano kati ya China bara na kisiwa cha Taiwan, akisema kutimiza muungano kamili wa China ni jukumu muhimu la kihistoria kwa Chama cha kikomunisti cha China, serikali ya China na wananchi wake, na kusisitiza kuwa kwenye mchakato wa kustawisha upya taifa la China, ni lazima na pia ni hakika muungano wa nchi utimizwe.

    Kwenye hotuba yake rais Xi ametoa wito kwa wachina wa kando mbili za mlangobahari wa Taiwan, kushirikiana katika kuhimiza ustawi wa taifa la China, kutafuta ufumbuzi wa Taiwan kwa "Mifumo miwili", kushikilia sera ya China moja, kuimarisha muunganiko wa kimaendeleo kati ya kando mbili, na kutimiza mapatano ya kina kati ya ndugu wa kando mbili, ili kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya kando mbili na hatimaye kutimiza muungano wa China kwa njia ya amani.

    Hotuba hiyo si kama tu imeweka bayana kuwa lengo la China kutimiza muungano kwa njia ya amani ni kusukuma mbele ustawi mpya wa taifa la China, na kwamba China bara inapenda kushirikiana na Taiwan katika kutafuta Ufumbuzi wa Mifumo miwili, bali pia imeonya kuwa kamwe China haitatoa nafasi yoyote kwa vitendo vya kuitenga Taiwan kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako