• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema China itaisaidia Afrika itimize kupata ongezeko la uchumi kwa kujitegemea na maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2019-01-04 18:25:45

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Ethiopia amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu mjini Addis Ababa,. Bw. Wang akizungumzia suala la madeni la Afrika amesisitiza kuwa China itaisaidia Afrika kutimiza ongezeko la uchumi kwa kujitegemea na kuleta maendeleo endelevu.

    Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa, ushirikiano kati ya China na Afrika siku zote umekuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano kati ya kusini na kusini, pia kwa ushirikiano wa kimataifa kwa nchi za Afrika. Kuisaidia Afrika ijiendeleze na kuwanufaisha waafrika ni moyo wa dhati wa China, ambao hautabadilika daima. Amesisitiza kuwa utoaji wa misaada na ushirikiano kati ya China na Afrika, umechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika, na pia kuboresha maisha ya waafrika. Bw. Wang Yi anasema:

    "Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, katika miaka miongo kadhaa iliyopita, China imeisaidia Afrika kujenga barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita elfu 10, reli zenye urefu wa zaidi ya kilomita 6,000, pamoja na mamia ya viwanja vya ndege, bandari na vituo vya kuzalisha umeme. China imetuma madaktari zaidi ya elfu 20 barani Afrika, kuwatibu watu zaidi ya milioni 200 wa huko. Vilevile China imepeleka watu wengi na vitu vingi katika kutoa mafunzo kwa maelfu ya mafundi katika sekta mbalimbali barani Afrika."

    Bw. Wang Yi ameeleza kuwa, shughuli hizo za China zimefurahiwa na nchi mbalimbali za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi za Afrika zimekumbwa na matatizo ya kifedha, hali ambayo imefuatiliwa sana na China. China ikiwa rafiki na ndugu mwema wa Afrika, inapenda kutoa misaada wakati waafrika wanapohitaji. Lakini linalowasikitisha watu ni kwamba, baadhi ya watu wanapotosha ukweli wa suala la madeni ya Afrika, hata wanajaribu kulihusisha na China, hali ambayo si kama tu halilingani na ukweli wa mambo, pia halikubaliki kwa nchi za Afrika. Bw. Wang akizungumzia suala hilo anasema:

    "Suala la madeni ya Afrika ni suala linalotokana na historia ndefu iliyopita, halitokani na hali ya hivi karibuni wala halikuzushwa na China. Jaribio la kuipaka matope China halitakubaliwa na waafrika, na ushirikiano kati ya China na Afrika hautaathiriwa na jaribio kama hilo. "

    Pia ameeleza kuwa uwekezaji na uchangishaji wa fedha wa China barani Afrika unafanyika kwa mujibu wa mtizamo wenye moyo wa dhati na kunufaishana uliotolewa na rais Xi Jinping wa China, ambao unaheshimu nia ya waafrika na kufuata mahitaji ya nchi mbalimbali Afrika, na si kujitafutia maslahi ya kisiasa, wala hauna masharti yoyote.

    Vilevile amesisitiza kuwa lengo la utatuzi wa suala la madeni ya Afrika ni kuhimiza Afrika itimize mapema uchumi wa kujitegemea na maendeleo endelevu. Kutokana na hali hii, China itashirikiana na Afrika katika kuharakisha hatua ya kutekeleza matokeo mbalimbali yaliyopatikana katika Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuongeza msukumo wa ndani wa kuhimiza uchumi wa Afrika. Wakati huo huo jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza ufuatiliaji na uwekezaji barani Afrika ili kusaidia na kuleta maendeleo kwa pamoja. Hayo ni mambo ambayo China inafanya hivi sasa, vilevile inatakiwa kuwa wajibu wa nchi nyingine duniani, haswa zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako