• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Magari binafsi yalazimika kubeba abiria kufuatia uhaba wa magari Moshi

  (GMT+08:00) 2019-01-04 20:51:10

  Wenye magari binafsi katika stendi kuu ya Mabasi Moshi walilazimika kutoa huduma za usafiri kwa wasafiri waliokosa usafiri kuhofia kupoteza ajira. Hii ni baada ya shida ya usafiri iliyotokana na mabasi mengi kujaa na hivyo watu wengi kukwama kusafiri. kuanzia saa 11 alfajiri idadi kubwa ya abiria ilishuhudiwa huku magari binafsi yakipakia abiria kwa Sh35,000 kwenda Dar es Salaam, lakini baadhi yakiwataka kushukia Chalinze mkoani Pwani.

  Kwa waliokuwa na upungufu wa nauli walikosa usafiri na miongoni mwao walieleza hofu yao ya kupoteza ajira zao.

  Baadhi ya abiria waliamua kurejea majumbani na wengine kuendelea kuwepo katika eneo hilo wakiwa na imani ya kupata usafiri utakaowafikisha wanakokwenda.

  Nauli pia ilipanda na kuwafanya wasafiri kulalamika. Uchunguzi uliofanywa na Radio China Kimataifa ulibaini kuwa magari binafsi yalitumia fursa ya uhaba wa mabasi kusafirisha abiria kwa kati ya Sh35,000 hadi 45,000 kwenda Dar es Salaam.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako