• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapata soko la sukari, alizeti na soya Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-01-04 20:52:57

    Serikali ya Uganda imesema wafanyabiashara wa nchi hiyo sasa wamepata soko la bure la sukari, alizeti na soya, baada ya makubaliano kati ya Tanzania na Uganda kufanyika Mutukula, mpakani mwa Uganda na Tanzania.

    Hayo yamewekwa wazi na wizara ya biashara ya Uganda ikionyesha kuwa bidhaa hizo zimeruhusiwa kuingia Tanzania.

    Miezi kadhaa iliyopita, Tanzania ilizuia uingizwaji wa baadhi ya bidhaa kutoka Uganda, jambo lililosababisha wafanyabiashara kuandamana nchini humo.

    Hata hivyo, kutokana na vikao kadhaa, Serikali ya Tanzania imekubali kutoa vibali vya uingizwaji wa bidhaa hizo kwa wafanyabiashara wa Uganda.

    Tanzania iliweka masharti hayo ya kuzuia wafanyabiashara kutoka Uganda kuingiza bidhaa hizo kutokana na kutuhumiwa kuingiza sukari toka nje, kisha kuzifungasha upya na kuzisafirisha tena kwenye masoko ya nje.

    Uhakiki wa pamoja umefanyika hivi karibuni, kwa ajili ya kupata uhakika wa chanzo cha alizeti na soya, ambapo imethibitika kuwa bidhaa hizo zinakidhi sheria za Shirikisho la Afrika Mashariki katika uasili wake, hivyo kukidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya mahitaji ya soko hilo la Afrika Mashariki.

    Hata hivyo, uhakiki huo umegundua kwamba mafuta ya nazi kwa ajili ya kupikia vyakula, hayakidhi viwango vya sheria za uasili za Shirikisho la Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako