• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo ya awali ya uchaguzi wa DRC yaahirishwa kutangazwa hadi wiki ijayo

    (GMT+08:00) 2019-01-06 16:53:34

    Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, Corneille Nangaa, utoaji wa matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini DRC, ambayo awali yalitarajiwa kutangazwa leo, umeahirishwa hadi wiki ijayo.

    Nangaa amesema ni vigumu kutangaza matokeo siku ya Jumapili, na ingawa wanaendelea vizuri lakini bado hawajakamilisha kila kitu. Amesisitiza kuwa wamepokea asilimia 45 hadi 48 tu ya kura kutoka nchi nzima.

    Kwenye uchaguzi huo uliofanyika tarehe 30 Disemba, mgombea wa muungano wa upinzani Lamuka, Martin Fayulu, amejitangazia ushindi licha ya CENI kutaka kuheshimiwa kwa sheria za uchaguzi ambazo zinaipa haki kamili tume hiyo ya kutangaza matokeo ya awali na ya mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako