• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Baiskeli ya Rwanda yaendelea na maandalizi kuelekea mbio za Gabon

  (GMT+08:00) 2019-01-07 08:56:43
  Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kuanza kwa mashindano ya kimataifa yam bio za baiskeli Gabon, timu ya Rwanda imeendelea na maandalizi chini ya kocha mkuu wake Sterling Magnell mjini Kigali.

  Ili kutetea ubingwa walioutwaa mwaka jana kwenye mashindano kama hayo kocha huyo amesema yafaa wachezaji waongeze bidii akisisitiza kuwa ushindani umeongezeka kutokana na kukua kwa mchezo huo duniani.

  Timu ya taifa ya Rwanda inaundwa na wachezaji sita wakiongozwa na Joseph Areruya ambaye aliibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mwaka jana.

  Mashindano ya Gabon kwa mwaka huu yanaanza Januari 21 na kumalizika januari 27.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako