• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuongeza nguvu katika kulinda haki miliki za kiubunifu

  (GMT+08:00) 2019-01-07 18:24:50

  Mkuu wa Idara Kuu ya Haki Miliki za kiubunifu ya China Bw. Shen Changyu amesema mwaka jana idadi ya hataza zilizoandikishwa nchini China ilizidi milioni 1.6, likiwa ni ongezeko la karibu asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2017. Amesema mwaka huu China itaongeza nguvu katika kulinda haki miliki za Kiubunifu, na kuzidisha ushirikiano wa kimataifa.

  Mkutano wa wakuu wa idara za haki miliki za kiubunifu umefanyika leo mjini Beijing. Akihutubia kwenye mkutano huo Mkuu wa Idara Kuu ya Haki Miliki za Kiubunifu ya China Bw. Shen Changyu amesema, mwaka jana nguvu ya jumla ya haki miliki za kiubunifu ya China ilipiga hatua mpya. Anasema,

  "Idadi ya hataza zilizoandikishwa nchini China (isipokuwa Hongkong, Macao na Taiwan ) ilifikia milioni 1.602, na kuongezeka kwa asilimia 18.1 ikilinganishwa na mwaka 2017. Wakati huo huo idadi ya hataza za kimataifa za PCT ilifikia elfu 55, likiwa ni ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na mwaka 2017."

  Bw. Shen amesema mwaka huu China itaendelea kuongeza nguvu ya kulinda hakimiliki za kiubunifu, kwa kuimarisha utafiti wa sheria husika na hatua za kulinda haki miliki za kiubunifu katika sketa mpya, kutunga na kutekeleza mpango wa ujenzi wa mfumo wa ulinzi, kuharakisha ujenzi wa utaratibu wa uendeshaji na jukwaa la kikazi, kutunga sera ya kulinda haki miliki za kiubunifu inayolingana na zama mpya, na kutafiti uwekezano wa kujenga kituo kikuu cha kulinda haki miliki za kiubunifu. Bw. Shen anasema,

  "Tutatekeleza vizuri matokeo ya mkutano wa ngazi ya juu wa pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' kuhusu haki miliki za kiubunifu, kuendelea kusukuma mbele mfumo wa Madrid wa kuandikisha chapa za kimataifa na makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa kuhusu hataza za kimataifa. Pia tutasaini makubaliano na shirika la kimataifa la haki miliki za kiubunifu kuhusu ujenzi wa kituo cha kuunga mkono uvumbuzi wa teknolojia, na kuongeza ushirikiano wa kimataifa."

  Bw. Shen amesisitiza kuwa, China inapaswa kusukuma mbele ujenzi wa utaratibu shirikishi wa kimataifa wenye uwiano na ufanisi katia kulinda haki miliki za kiubunifu, na kushikilia kanuni ya pande nyingi. Anasema,

  "Tunapaswa kushikilia ushirikiano, kusukuma mbele ushirikiano wa haki miliki za kiubunifu katika pendekezo la 'Ukanda Mmoja na Njia Moja', na ushirikiano kati ya China na Marekani, Ulaya, Japan, Korea ya Kusini, nchi za BRICS, nchi za kusini mashariki mwa Asia, na nchi nyinginezo, ili kujenga utaratibu mpya wa kimataifa katika kulinda haki miliki za kiubunifu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako