• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa mihogo Tanga walalamikia hasara

    (GMT+08:00) 2019-01-07 18:47:02

    Wakulima mihogo wa Mkoa wa Tanga wamo wameutaja mwaka wa 2018 kuwa mwaka wenye machungu mengi baada ya kupata hasara kubwa kwenye kilimo chao. Wakulima hao wanasema mwaka huo walikosa soko la mihogo waliyozalisha kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote baada ya kuhakikishiwa soko bila mafanikio. Takriban kila kijiji mkoani Tanga, isipokuwa maeneo ya milima ya Usambara katika wilaya za Korogwe, Lushoto na Mkinga, wakulima walilima mihogo kwa wingi baada ya kuahidiwa soko na bei nzuri. Hamasisho la kulima mihogo lilianzishwa na viongozi wa serikali na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali wakiwaeleza wakulima kwamba kuna soko kubwa kutoka nje ya nchi. Hamasa hiyo ilisababisha wananchi wengi kujiingiza katika kilimo cha mihogo. Wengine walienda mbali na kuamua kukopa kwenye taasisi za fedha kama benki, vikoba na saccos kwa matarajio ya kuzirejesha baada ya kuuza kwa faida. Katika baadhi ya mashamba, zao hilo limeharibika kwa kugeuka miti kutokana na kutovunwa kwa wakati kwa sababu wakulima hawana soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako