• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NFRA yatakiwa kuweka mikakati ya kununua mazao ya wakulima

    (GMT+08:00) 2019-01-07 18:50:28

    Wakala wa taifa wa hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na bodi ya nafaka na mazao nchini Tanzania zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuainisha jinsi watakavyonunua mazao ya wakulima nchini humo.NFRA imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbali mbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.Waziri wa kilimo wa Tanzania Japheth Hasunga amesema wamekuwa wakihamasisha wakulima kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara na watahakikisha kuwa wakulima hao wanauza mazao yao kwa bei ya faida.Waziri pia amepongeza NFRA kwa kujenga kujenga maghala mengine zaidi akisema yatasaidia kuhifadhi chakula cha kutosha nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako