• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya SportPesa yaiva

  (GMT+08:00) 2019-01-08 09:39:11
  Ratiba ya michuano ya SportPesa imetolewa jana huku michuano hiyo ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 22 hadi 27 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Ratiba hiyo ambayo mzimu huu ni mashindano ya tatu mfululizo kufanyika, imewekwa hadharani na waandaaji wa michuano hiyo kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa .

  Yanga ya Tanzania itaumana na Kariobangi Sharks ya Kenya, mabingwa watetezi Gor Mahia ya Kenya wataumana uso kwa uso na Mbao FC ya Tanzania, huku mtanange wa mwisho hatua ya robo fainali utapigwa kati ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba sports club na AFC Leopards.

  Mchezo wa nusu fainali utapigwa Januari 25 huku kumtafuta mshindi wa tatu utachezwa Januari 27 majira ya mchana na fainali kupigwa jioni yake.

  Bingwa wa michuano hiyo atakutana na timu ya Everton kutoka ligi kuu ya Uingereza (EPL)

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako