• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi wa kisiasa na kibiashara wa China na Marekani wataka nchi hizo mbili ziendelee kukuza ushirikiano

  (GMT+08:00) 2019-01-09 17:02:38

  Tafrija ya mwaka 2019 ya shirikisho kuu la wafanyabiashara wa China nchini Marekani ilifanyika tarehe 7 usiku nchini Marekani. Viongozi wa kisiasa na kibiashara wa China na Marekani kwa kauli moja wameona kuendelea kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, ni jambo muhimu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao na hata kwa amani na usalama wa duniani.

  Tafrija hiyo iliwaleta pamoja karibu watu 450 akiwemo balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai, na mwenyekiti wa bodi ya shirika la uwekezaji la Starr la Marekani Bw. Maurice Greenberg. Balozi Cui alipohutubia tafrija hiyo amesema, China itaendelea kujitahidi kuongeza ushirikiano na Marekani kwa kufuata kanuni ya kunufaishana na kupata mafanikio ya pamoja, na kutatua migongano kwa njia ya kuheshimiana, na kuendeleza uhusiano wenye uratibu, ushirikiano na utulivu kati ya nchi hizo mbili. Anasema,

  "China itashirikiana vizuri na Marekani, ili kujenga uhusiano wenye nguvu na utulivu. Uzoefu wa miaka 40 iliyopita umethibitisha kuwa sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China na hali ya kawaida na maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya China na Marekani zinanufaisha nchi hizo mbili na dunia nzima. Historia imetuonesha kuwa, kwa China na Marekani, ushirikiano unaleta manufaa ya pamoja, na mivutano inaleta hasara kwa pande zote."

  Mkuu wa shirikisho la wafanyabiashara wa China nchini Marekani ambaye pia ni mkuu wa tawi la Benki ya China nchini Marekani Bw. Xu Chen, amesema kutokana na matatizo na changamoto zinazokabili uhusiano kati ya China na Marekani, shirikisho hilo litajitahidi kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa uwekezaji na biashara kati ya nchi hizo mbili. Anasema,

  "Ingawa uhusiano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani umekabiliwa na mivutano mbalimbali, tumekutana hapa tukieleza matumaini yetu. Changamoto zinazotukabili hazijapunguza imani na nia yetu ya kuimarisha mazungumzo na kupanua ushirikiano wa uwekezaji na biashara."

  Viongozi wengi wa kisiasa na kibiashara wa Marekani waliohudhuria tafrija hiyo wamesema, wakati wa kuadhimisha miaka 40 tangu Marekani na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo bado zinahitajiana, na zinapaswa kuendelea kushirikiana ili kuhimiza amani na usalama duniani. Mwenyekiti wa bodi ya shirika la uwekezaji la Starr la Marekani ambaye pia ni mtendaji mkuu wa shirika hilo Bw. Maurice Greenberg, ameeleza imani yake kubwa kuhusu mustakbali wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Katika tafrija hiyo amepewa heshima ya "balozi wa mawasiliano kati ya China na Marekani". Anasema,

  "Naona furaha na fahari kwa kupata heshima hiyo. Ingawa uhusiano kati ya Marekani na China unapanda na kushuka, mwelekeo wa kupanda utashinda changamoto, huku mwelekeo wa kushuka utazuiliwa. Nchi hizi mbili zinapaswa kuendelea kushirikiana, ili kuhimiza amani na usalama wa dunia kwa pamoja."

  Rais wa zamani wa Marekani Bw. Jimmy Carter ametoa salamu za pongezi kwa tafrija hiyo, akisema wakati uhusiano kati ya Marekani na China unakabiliwa na changamoto ambayo haijawahi kutokea, nchi hizo mbili zinapaswa kuongeza mawasiliano zaidi katika uchumi, elimu na utamaduni, ili kusukuma mbele uhusiano kati yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako