• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: KOMBE LA LIGI: Manchester City yaifumua Albion 9 Nunge

  (GMT+08:00) 2019-01-10 10:10:28

  Mchezo mwingine wa nusu fainali ya kombe la ligi Uingereza maarufu kama Carabao ulipigwa usiku wa kuamkia leo kati ya timu ya Manchester City ilipovaana na Burton Albion.

  Unaweza kudhani ni mechi ya mpira wa kikapu ama mkono yaani Basketball ama Netball lakini ni mchezo wa soka pale ambapo Man City imeifumua bila huruma Albion kwa jumla ya magoli 9-0.

  Akizungumza mara baada ya mchezo huo, kocha wa Man City Pep Guardiola amesema, hawakudharau mechi hiyo licha ya mashabiki kumlaumu kutomuanzisha mchezaji Phil Foden katika kikosi cha kwanza, lakini anaamini kila mchezaji anajukumu la kutafuta ushindi wawapo uwanjani na si vinginevyo, hivyo anatoa nafasi kwa kila mchezaji aliyesajiliwa kuitumikia timu kwenye mechi tofautitofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako