• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo mazuri ya mwisho kupatikana kutokana na juhudi za pamoja za China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-01-10 17:00:17

    Mazungumzo ya ngazi ya naibu mawaziri kati ya China na Marekani kuhusu suala la uchumi na biashara yalifungwa jana mjini Beijing. Haya ni mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili kwa ajili ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili nchini Argentina.

    Kwenye mazungumzo hayo, China na Marekani zimefikia makubaliano kwamba, China itanunua zaidi mazao ya kilimo na nishati kutoka Marekani. Makubaliano hayo pia yanalingana na mahitaji ya wateja na maendeleo yenye ubora zaidi ya uchumi nchini China. Marekani pia imeweka masharti ya kuitaka China kufafanua ratiba kamili ya kuongeza manunuzi hayo. Lakini kwa kweli, kiwango cha mauzo ya bidhaa hizo za Marekani nchini China kinategemea ubora wake, na kama zinaweza kupendwa na wateja wa China.

    Kwenye mazungumzo hayo, Marekani pia imetaja "marekebisho ya miundo" ya China. China kamwe haitapokea masharti ya kurekebisha mifumo ya kitaifa, kiusalama na kimawazo, lakini marekebisho katika sekta za uchumi na biashara haswa ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu yametekelezwa nchini China.

    Mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani umeendelea kwa zaidi ya miezi 9. Sasa pande hizo mbili zimepiga hatua katika mazungumzo ya ngazi ya naibu mawaziri, kutokana na sababu muhimu kwamba, mvutano huo umeathiri pande hizo zote na hata dunia nzima. Tangu katikati ya mwezi Oktoba mwaka jana , nchini Marekani soko la hisa lilishuka kwa mfululizo, na pengo la biashara lilifikia dola bilioni 50.5 za kimarekani ambao lilivunja rekodi tangu miaka 6 iliyopita. Wakati huo huo, kielezo cha PMI cha uzalishaji wa viwanda nchini China kwa mwezi uliopita kilishuka mpaka chini ya mstari kati ya ustawi na kudhoofika.

    Kwa dunia nzima, ongezeko la thamani ya biashara duniani kwa mwaka jana linaweza kushuka kwa asilimia 0.3. Benki ya dunia hivi karibuni imeshusha makadirio yake kuhusu ongezeko la uchumi wa dunia katika mwaka huu na mwaka ujao kwa asilimia 0.1. Gazeti la New York Times linaona mvutano wa kibiashara umeleta wasiwasi kwa soko la fedha, na hasara halisi wa kiuchumi.

    Kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China na Marekani, nchi hizo mbili zitamaliza mazungumzo ndani ya siku 90, na sasa siku 40 zimepita. Hivyo pande hizo mbili zinapaswa kuharakisha mchakato huu ili kupata matokeo mazuri.

    Kutokana na utatanishi wa mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani, China imeonesha udhati na kufanya juhudi kubwa kadiri iwezavyo, lakini matokeo mazuri ya mwisho yatapatikana kutokana na juhudi za pamoja za nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako