• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kutekeleza vizuri sera tulivu ya sarafu

    (GMT+08:00) 2019-01-10 19:15:19

    Mkuu wa benki kuu ya China Bw. Yi Gang, amesema benki hiyo itaendelea kutekeleza sera tulivu ya sarafu, ili kuongeza uwezo wa utoaji wa huduma za mashirika ya fedha kwa uchumi halisi.

    Bw. Yi Gang amesema kwa mujibu wa Mkutano wa kazi ya uchumi wa Kamati Kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, benki hiyo itazidi kuimarisha marekebisho ya hali inayokwenda tofauti na mkondo wa uchumu, na kupunguza vizuizi dhidi ya utoaji wa mikopo; wakati huo huo, itaendelea na mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa, kuongeza nguvu katika kuunga mkono uchumi halisi ikiwemo viwanda vya watu binafsi, mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati. Katika kipindi kijacho, China vilevile itazidi kuboresha utaratibu wa sera za fedha, kuanzisha utaratibu wa uhamasishaji kwa benki, na kuongeza nguvu katika kuunga mkono uchumi halisi.

    Bw. Yi Gang pia ameeleza kuwa benki hiyo itachukua vyombo mbalimbali vya sera za kiuchumi ili kulenga kihalisi mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati, na kuzisaidia kampuni za watu binafsi kwa njia ya utoaji wa mikopo, dhamana na hisa. Wakati huo huo itaendelea kuyahimiza mashirika ya fedha kuongeza nguvu kutoa huduma kwa kampuni za watu binafsi, na mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako