• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa Tumbaku wakosa soko Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-01-10 19:46:39
    Wakulima wa tumbaku mkoani Katavi nchini Tanzania wanakabiliwa na hali ngumu baada ya kukosa soko la zao hilo kutokana na kampuni zilizokuwa zikinunua kupunguza kiwango cha kununua kwenye vyama vya wakulima vya msingi.

    Miaka mitatu iliyopita kampuni hizo zilikuwa zikinunua kwenye vyama hivyo kilo milioni 16, lakini katika msimu huu wa mavuno kampuni hizo zimenunua kilo milioni sita tu.

    Akizungumza na wadau wa kilimo mkoani humo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mathew Mtigumwe, alisema kutokana na hali ilivyo, serikali imeamua kutafuta masoko mengine ya zao hilo.

    Alisema wizara imeiagiza Bodi ya Tumbaku iende moja kwa moja kwenye nchi ambazo zinatumia sana tumbaku ili kutafuta soko la tumbaku lengo likiwa kuwasaidia wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako