• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kufungua mlango zaidi katika sekta ya uzalishaji

  (GMT+08:00) 2019-01-11 17:18:35

  Waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Miao Wei, amesema China itaboresha mazingira kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya uzalishaji, kwa kuendelea kupunguza ushuru na gharama, na kufungua mlango zaidi, ili kuharakisha maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta hiyo.

  Mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za kiuchumi uliofanyika hivi karibuni, uliweka kipaumbele katika kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya sekta ya uzalishaji, na kuagiza kushirikisha sekta ya kisasa ya uzalishaji na sekta ya huduma kwa kina, ili kuijenga China iwe nchi yenye nguvu kubwa ya uzalishaji. Waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Miao Wei anaona kuwa, China ina soko kubwa, muundo kamili wa sekta, uwezo wa uvumbuzi unaoongezeka kwa mfululizo, miundombinu bora na mazingira mazuri ya biashara, kwa hiyo ina uwezo wa kutosha wa kukabiliana na changamoto za nje. Anasema,

  "Tunapaswa kukamilisha mifumo mbalimbali ya vigezo, sera na tathmini, kuondoa vizuizi vya kugeuza vitu vilivyovumbuliwa kuwa matoleo halisi ya viwanda, kuendelea kurekebisha mwundo, na kubadilisha njia ya kuendeleza sekta ya uzalishaji. Aidha katika miaka miwili ijayo, tutakusanya raslimali katika kusaidia mikoa ambayo haijatimiza lengo la kuondoa uwezo wa uzalishaji usiohitajika."

  Bw. Miao amesema ili kutoa mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya kampuni, mwaka huu serikali ya China itaendelea kuongeza ufanisi wa kazi, na kupunguza ushuru na gharama. Aidha, itaendelea kufungua mlango, na kutekeleza sera ya kuwapa wawekezaji wa nje hadhi sawa na wawekezaji wa ndani, isipokuwa shughuli maalumu zilizoorodheshwa. Anasema,

  "Baadaye tutatoa hatua kubwa zaidi ya kupunguza ushuru kwa sekta ya uzalishaji, na pia tutahamasisha serikali katika ngazi mbalimbali kupunguza ada husika za kampuni."

  Umuhimu wa miundombinu ya upashanaji habari wa simu ya mkononi kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini China umedhihirika. Bw. Miao amesema, teknolojia ya 5G itakuwa injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa kidata na sekta nyingine mbalimbali. Mwishoni mwa mwaka jana, wizara ya viwanda na teknolojia ya habari ya China ilitoa kibali cha kujaribu 5G kwa kampuni tatu kuu ya upashanaji habari. Anasema,

  "Kwa kufuata mpango uliowekwa na mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za kiuchumi, tunaharakisha hatua ya kutumia teknolojia ya 5G kibiashara. Tunakadiria kuwa hadi kufikia robo ya pili ya mwaka huu, simu na Pad za 5G zitapatikana nchini China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako