• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema kazi ya chombo cha safari ya anga za juu Chang'e-4 imefanyika kwa mafanikio

  (GMT+08:00) 2019-01-11 19:00:08

  China imetangaza kuwa kazi ya chombo cha safari ya anga za juu cha nchi hiyo Chang'e-4 ya kupiga picha kwenye sayari ya mwezi imefanyika kwa mafanikio.

  Chombo hicho kimepiga picha katika eneo la juu la sayari ya mwezi baada ya kutua kwa mafanikio pembezoni mwa sayari hiyo.

  Idara ya taifa inayosimamia anga za juu ya China imetoa picha zilizopigwa kwa kutumia kamera iliyowekwa kwenye chombo hicho. Picha hizo zilitumwa duniani kupitia satelaiti ya Queqiao iliyoko umbali wa kilomita zaidi ya laki 4 kutoka sayari ya dunia.

  Mradi wa anga za juu wa China uliopewa jina la Chang'e ulianza mwaka 2004, na unajumuisha kuzunguka na kutua katika sayari ya mwezi na kuleta sampuli duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako