• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Klabu Bingwa Afrika: Simba yawatuliza JS Saoura, Al Ahly yapeta

  (GMT+08:00) 2019-01-14 08:49:38

  Simba Sports Club ya Tanzania imeanza vyema mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya JS Saoura ya Algeria kwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 3-0.

  Mechi nyingine ya kundi hilo ilikuwa kati ya Al Ahly ya Misri ilipoikaribisha AS Vita ya DRC katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria. Al Ahly imebuka na ushindi wa magoli 2-0.

  Kwa matokeo hayo, Simba ya Tanzania inaongoza kundi hilo la D, ikiwa na alama 3 na magoli 3, inafuatiwa na Al Ahly yenye alama 3 na magoli 2, AS Vita imekamata nafasi ya tatu kwa kutokuwa na alama wala goli la kufunga na JS Soura yenyewe inakamata mkia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako