Watu saba wamefariki leo baada ya ndege aina ya Boeing 707 kuanguka katika mji wa Karaj, kaskazini mwa Iran.
Shirika la Habari la ISNA limemnukuu mkuu wa kituo cha dharura cha Iran Pir Hossein Kolivand akisema, ndege hiyo ya mizigo iliyokuwa na watu 16 ndani ilianguka kwenye eneo la makazi, kilomita 45 kutoka mji mkuu wa Tehran.
Taarifa iliyotolewa na idara ya uhusiano wa umma ya jeshi la Iran imesema, ndege hiyo, mali ya Kyrygyzstan, ilitokea mji mkuu wa nchi hiyo, Bishkek, na ilikuwa imebeba shehena ya nyama kupeleka Iran.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |