• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Uganda mbioni kupunguza gharama za umeme

  (GMT+08:00) 2019-01-14 19:58:53

  Mamlaka ya kuthibiti umeme nchini Uganda ERA imesema inaweza kutekeleza mapendekezo ya gharama ya umeme kuwa senti 5 za Marekani kwa kilowati moja lakini itafanya hivyo polepole.

  Mkuu wa mawasiliano kwenye mamlaka hiyo Julius Wandera, amesema hata hivyo watumiaji wa umeme wa wastani watahitajika kutumia kiwango kikubwa cha umeme ili kuipata kwa senti 5.

  Aidha amesema lazima kuwe na ongezeko la mahitaji ya kawi kama vile taasisi za elimu kuanza kupika kwa kutumia stima.

  Wiki iliopita mnadhimu mkuu wa serikali Ruth Nankabirwa, alisema baraza la mawaziri tayari limeidhinisha upunguzaji wa gharama za umeme kwa viwanda vidogo vinavyofanya shughuli za kuoneza ubora wa bidhaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako