• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Uzalishaji wa korosho mkoani tanga, washuka

    (GMT+08:00) 2019-01-14 19:59:11

    Uzalishaji wa zao la korosho mkoani tanga, umeshuka kutoka tani 1,712 zilizovunwa mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 1,381 kwa mwaka 2017/018.

    Mrajisi wa Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Jacqline Senzige anasema sababu zilizoshusha uzalishaji wa zao hilo ni pamoja na mvua za mfululizo zilizonyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha maua kudondoka na kuozesha matunda.

    Sababu nyingine kwa mujibu wa Senzige ni mwitikio mdogo wa wakulima kulipokea zao hilo ambalo lilikuwa geni kwao hasa kwa wakulima wa Wilaya ya Handeni na ukosefu wa elimu ya faida ya zao hilo kwa wananchi.

    Kutokana na changamoto hizo, aliwashauri maofisa ugani waendelee kutoa elimu ya faida za kilimo cha korosho kwa mkulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako