• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mamlaka ya chakula na dawa Tanzania kulinda soko la ndani

  (GMT+08:00) 2019-01-14 20:00:04

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini nchini Tanzania imeeleza kuwa, itaendelea kulinda soko la ndani la bidhaa za vyakula ,dawa, na vipodozi kwa kuimarisha huduma kwenye mipaka yote nchini ikiwemo mpaka wa Namanga, Mkoani Arusha.

  Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny amesema udhibiti katika mipaka hiyo ni unalenga kuhakikisha kuwa bidhaa bora, salama na zenye ufanisi pekee ndiyo zinaingia nchini ili kulinda afya ya wananchi.

  Mpaka wa Namanga ni moja ya mipaka ambayo tayari imeanza kufanya kazi kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa upande mmoja tu wa Nchi (One Stop Boder Post-OSBP) ambapo bidhaa inaingia na kukaguliwa kwa pamoja na wakaguzi wa nchi mbili (Tanzania na Kenya) ili kupunguza muda wa wadau kukaa mpakani kwa muda mrefu kwa ukaguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako