• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa wito wa kuhakikisha ukuaji wa uchumi ndani ya kiwango kinachofaa

    (GMT+08:00) 2019-01-15 09:19:25

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa wito wa kufanya juhudi kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa ndani ya kiwango kinachofaa.

    Jana Bw Li aliendesha mkutano wa baraza la serikali ya China, ambapo washiriki wamejadili mswada wa taarifa ya kazi ya serikali pamoja na kazi ya kiuchumi katika kipindi cha robo ya kwanza cha mwaka 2019. Bw. Li amesema China itakabiliwa changamoto nyingi na hali ya maendeleo yenye utatanishi zaidi kwa mwaka huu.

    Amehimiza kufanya juhudi za kudumisha uwiano kwenye sekta za ukuaji wa uchumi, kuhimiza mageuzi, kurekebisha miundo, kuboresha maisha ya wananchi na kuepusha hatari.

    Mbali na hayo Bw Li Keqiang pia ameagiza kuimarisha usimamizi kwa wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China kwenye ngazi zote za serikali, na kutekeleza maagizo ya Rais Xi Jinping kuhusu usimamizi wa chama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako