Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang hapa Beijing amekutana na rais Sauli Niinisto wa Finland.
Bw. Li amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na Finland kuhimiza nchi hizo mbili kupata maendeleo mengi mapya na kutia nguvu mpya katika uhusiano kati ya pande mbili. Pia amesema China inapenda kuzidisha ushirikiano na Finland katika usafirishaji wa mizigo, huduma na teknolojia na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo yasiyochafua mazingira na nishati safi.
Rais Niinisto amesema, Finland inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya kampuni za nchi mbili hasa kati ya kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati na China, kuimarisha ushirikiano wa mabadiliko ya hali ya hewa, ubunifu wa teknolojia na nishati safi na kulinda mfumo wa pande nyingi wa kibiashara kwa pamoja.
Habari nyingine zinasema, spika wa bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu leo pia amekutana na rais Niinisto.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |