• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: AFCON U17- Viwanja, Hospitali na Hoteli zakaguliwa

  (GMT+08:00) 2019-01-16 08:36:09

  Mtendaji mkuu wa kamati ya ndani inayosimamia maandalizi ya michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 inayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania mwaka huu, Leslie Liunda amesema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yapo katika hatua nzuri.

  Liunda ameeleza kuwa tayari awamu ya kwanza ya ukaguzi kutoka kwa kamati maalum ya shirikisho la soka Afrika (CAF) umefanyika na wametoa maelekezo juu ya vitu vya kufanya kuelekea michuano hiyo.

  Viwanja ambavyo vimepangwa kutumika katika michuano hiyo ni uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Chamazi. Huku jumla ya timu 8 ikiwemo mwenyeji Tanzania zitashiriki michuano hiyo. Mataifa mengine ni Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako