• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je, Uingereza inaelekea wapi baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya?

    (GMT+08:00) 2019-01-16 17:16:06

    Baraza la chini la bunge la Uingereza limepiga kura juu ya makubaliano ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya yaliyofikiwa kati ya waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May na Umoja wa Ulaya, na kuyakataa kwa kura 431 za hapana na 202 za ndiyo.

    Matokeo hayo hayastaajabishi watu, kwani kabla ya kufanyika kwa upigaji kura huo, vyombo vya habari duniani vilikadiria kuwa kuna uwezekano mkubwa wa makubaliano hayo kukataliwa. Lakini kura za hapana zinazidi zile za ndio kwa 230, pengo hilo kubwa limezidi matarajio ya watu, hali ambayo imeonesha kuwa sera zinazotekelezwa na Bi. Theresa May ambazo zinalenga kudumisha uhusiano wa karibu kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya zimeshindwa, na kuufanya mchakato wa Uingerza wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya kukabiliana na changamoto kubwa na chaguo gumu zaidi tokea Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

    Je, Uingereza itaelekea wapi baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya? Mwenyekiti wa Baraza la mambo ya Ulaya Bw. Donald Franciszek Tusk amesema, endapo hakuna uwezekano wa kufikia makubaliano, na wala hakuna mtu anayetarajia Uingereza itajiondoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano, je nani ana ushupavu wa kutoa pendekezo la pekee juu ya ufumbuzi wa suala hilo? Kwa kweli pendekezo hilo litaifanyaUingereza ibaki kwenye Umoja wa Ulaya. Upo uwezekano kama huo, lakini inahitaji wanasiasa wa Uingereza kuwa na ushupavu wa kurejesha ombi la Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. Bila shaka uamuzi huo utaleta hatari kubwa ya kisiasa.

    Kwa maoni ya waangalizi wengi wa kimataifa, uamuzi wa Uingereza wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya ni kosa kubwa, ambao si kama tu utadhoofisha hadhi ya nchi za magharibi duniani, bali pia utaleta hali isiyoweza kutabirika kwenye mustakabali wa uchumi wa Uingereza, na pia kutingisha hadhi ya mji wa London ukiwa kituo cha fedha duniani. Je, kujiondoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya ni kosa kubwa au ni fursa ambayo haijawahi kutokea katika historia? Hili ni chaguo litakalofanywa kwa uwajibikaji na wanasiasa wa Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako