• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China kuhimiza mchakato wa muungano wa taifa mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-01-16 18:31:06

    Msemaji wa ofisi ya baraza la serikali ya China inayoshughulikia mambo ya Taiwan Bw. Ma Xiaoguang amesema, mwaka huu China ina uwezo wa kushinda hatari na changamoto mbalimbali, na kuhimiza mchakato wa amani na umoja wa taifa.

    Bw. Ma amesema, mwaka 2019 ni maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China kuasisiwa, pia ni maadhimisho ya miaka 40 tangu kamati ya kudumu ya bunge la umma la China kutoa "Ujumbe kwa Ndugu wa Taiwan". Mwanzoni mwa mwaka huu, rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba iliyozungumzia kufanya juhudi pamoja kwa ajili ya kutimiza ustawi wa taifa na kuhimiza muungano wa amani wa taifa, na kutoa mwongozo wa msingi wa kushughulikia mambo kuhusu Taiwan katika zama mpya.

    Pia ameongeza kuwa, ingawa uhusiano kati ya pande mbili za mlango wa bahari wa Taiwan bado unakumbwa na changamoto mbalimbali, wanaojaribu kuifanya Taiwan ijitenge kutoka China wataendelea kufanya uchokozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako