• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uingereza yanusurika kura ya kutokuwa na imani kwa wingi mdogo

    (GMT+08:00) 2019-01-17 09:26:14

    Serikali ya waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May imenusirika kwenye upigaji kura wa kutokuwa na imani kwenye baraza la makabwela la bunge la Uingereza, na kukwepa kuitisha uchaguzi mkuu wa mapema.

    Hoja ya upigaji kura ya kutokuwa na imani na serikali iliwasilishwa na kiongozi wa chama cha Labor Bw. Jeremey Corbyn na kupata kura 306 za ndio na kura 325 za hapana, na serikali kunusurika kwa kura 19 tu.

    Hii inamaanisha kuwa Bibi May ataendelea kuomba Uungaji mkono wa bunge kuendelea na mpango wake wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya baadaye mwaka huu. Anatarajiwa kurudi tena bungeni jumatatu na mpango mwingine, baada ya mpango wake wa awali kushindwa vibaya kwenye upigaji kura.

    Bw. Corbyn amesema mawaziri wote wakuu waliopita waliokuwa kwenye hali kama ya Bibi May wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi wa mapema. Lakini Bibi May amesema uchaguzi mkuu ungekuwa ni jambo baya sana kwa Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako