• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa rais wa China akutana na rais wa Misri

    (GMT+08:00) 2019-01-17 10:10:34

    Mjumbe maalumu wa rais wa China Bw. Yang Jiechi amekutana na rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri mjini Cairo.

    Bw. Yang Jiechi amekabidhi salamu za rais Xi Jinping wa China kwa rais al Sisi, na kusema uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri umeendelezwa vizuri katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na juhudi za marais wa nchi hizo mbili, amesema ziara yake hii inalenga kuimarisha makubaliano yaliyofikiwa na marais hao.

    Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kudumisha mwelekeo wa mawasiliano kati ya viongozi, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na kuungana mikono katika masuala yanayohusu maslahi makuu na ufuatiliaji wa upande mwingine. Pia amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano wa kivitendo chini ya utaratibu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuwanufaisha wananchi wao.

    Rais al-Sisi amesema Misri na China ni marafiki wakubwa na Misri inatilia maanani hadhi ya kimataifa ya China na kupenda kushirikiana na China katika kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Ameongeza kuwa Misri itatumia fursa ya kuwa mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika kuhimiza ushirikiano kati ya Afrika na China na kati ya Misri na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako