• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yajaribu kuondoa mzizi wa ugaidi kwa mafunzo ya ajira mkoani Xinjiang

  (GMT+08:00) 2019-01-17 12:23:59

  Waandishi wa habari waliohudhuria awamu ya 7 ya "Safari ya Watu Mashuhuri wa Nchi za Njia ya Hariri nchini China" hivi karibuni walitembelea kituo cha mafunzo ya ajira cha mji wa Kashi kusini mwa mkoa unaojiendesha wa kabila la wauyghur wa Xinjiang. Wageni hao kutoka Uturuki, Misiri, Afghanistan, Pakistan, Bangladesh na Sri Lanka walibadilishana maoni kwa kina na wanafunzi na walimu wa huko.

  Uzoefu wa mapambano dhidi ya ugaidi umethibitisha kuwa msimamo mkali wa kidini huleta ugaidi, ili kuondoa ugaidi, ni lazima kung'oa mzizi wake wa kimawazo. Hivi sasa njia muhimu ya mkoa wa Xinjiang kupambana na ugaidi ni kutoa mafunzo ya ajira kwa watu wanaoathiriwa na msimamo mkali wa kidini ambao hawana makosa makubwa.

  Mwenyekiti wa shirikisho la waandishi wa habari la Uturuki Bw. Misket Dikmen anaona kuna maana kubwa kwake kupata fursa ya kutembelea kituo hicho. Anasema,

  "Kuna maoni mengi kuhusu vituo vya aina hiyo mkoani Xinjiang. Moja ni kwamba madhumuni ya kuvijenga ni kuwafanya wauyghur wawe kama wahan. Lakini ukweli ni kwamba watu wamekuja hapa kwa hiari, ili kujifunza elimu za kazi, na wao wote wanaridhika na masomo na maisha ya hapa."

  Waandishi hao wa habari walibadilishana maoni na wanafunzi wa kituo hicho. Mhariri mkuu wa Gazeti la Kandahar Orband la Afghanistan Bw. Abdul Matin Amiri anasema,

  "Zamani kutokana na baadhi ya ripoti, nilidhani serikali ya China imewafunga watu hao na kuwalazimisha kupewa mafunzo. Lakini hali niliyoiona hapa ni tofauti, na hapa ni shule tu. niliwahoji baadhi ya wanafunzi, wanafurahia kupata elimu za kazi. Na kitu muhimu zaidi ni kuwa wameachana na msimamo mkali."

  Katika darasa la muziki, wanafunzi waliovaa mavazi ya kikabila wanaimba na kucheza ngoma kwa furaha, huku katika kiwanja cha michezo, watu wakicheza mipira ya aina mbalimbali. Mwendeshaji wa FM98 ya Pakistan Bw. Tassawar Zaman Babar anasema,

  "Baada ya kutembelea kituo hicho, nataka kuipongeza China kwa juhudi zake za kuondoa mawazo makali. Madhumuni ya kujenga vituo hivyo ni kuongeza mawasiliano kati ya watu, na kuwaambia kuheshimiana na kupendana, na kutopinga taifa, wananchi na makabila mengine."

  Kuondoa ugaidi na misimamo mikali ni lengo la dunia nzima, na pia ni changamoto kubwa ya dunia nzima. Waandishi hao wa habari wamesema, vituo vya kutoa mafunzo ya ajira ni njia bora iliyobuniwa na China, na inastahili kuigwa na nchi nyingine. Bw. Amiri anasema,

  "Afghanistan inaathiriwa vibaya na mashambulizi ya kigaidi. Kama ikiiga mfano wa China, na kuanzisha vituo hivyo ili kubadilisha mawazo ya watu waliozusha mashambulizi hayo, naona hali itabadilika."

  Mhariri wa jarida la Al-ahram Ektassdy la Misri Bw. Samia Fakhry Mansour anasema,

  "Hili ni jaribio zuri ambalo linastahili kuigwa na nchi nyingine. Linaweza kuwaokoa watu wanaoanza kuathiriwa na misimamo mikali kwa wakati."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako