• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 18 wafariki katika ajali ya basi magharibi mwa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-01-17 18:42:58

    Polisi nchini Ethiopia imesema, watu 18 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la abiria kupinduka magharibi mwa Ethiopia hapo jana.

    Mkuu wa polisi wa usalama barabarani kanda ya Wollega Mashariki Bw. Turumsa Solomon amesema, abiria 33 waliokuwa ndani ya basi hilo wanapatiwa matibabu, huku 10 kati yao wakiwa wameumia vibaya. Ameeleza wasiwasi wake kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

    Inasemekana kuwa tatizo la kiufundi ndio chanzo cha ajali hiyo ambayo imetokea siku chache baada ya ajali nyingine ya barabarani kusababisha vifo vya watu 17 nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako