• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Afrika wakutana Addis Ababa kujadili hali ya DRC baada ya uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2019-01-18 08:40:59

    Viongozi wa Afrika wamekutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, kujadili njia za kutatua masuala yaliyopo baada ya uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Mkutano huo ulioendeshwa na rais Paul Kagame wa Rwanda, umehudhuriwa na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed, rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na rais Yoweri Museveni wa Uganda.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo rais Kagame amewapongeza viongozi wa SADC kwa juhudi zao katika kukabiliana na mgogoro baada ya uchaguzi nchini DRC, na kusisitiza haja kwa waafrika kukutana na kutafuta kwa pamoja ufumbuzi wa matatizo yao.

    Naye mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ametoa wito kwa wadau wote nchini DRC kuchukua hatua za kuimarisha demokrasia na kulinda amani kufuatia kutolewa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako