• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RUGBY: Timu ya taifa ya Rugby ya Kenya yapata nahodha mpya

    (GMT+08:00) 2019-01-18 08:52:18
    Jacob Ojee ameteuliwa kuwa nahonda wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya almaarufu kama Mashujaa.

    Mashujaa itaondoka kesho jumamosi kushiriki mashindano mawili ya raga ya dunia katika miji ya Hamilton New Zealand na Sydney Australia.

    Ojee kutoka klabu ya KCB aliwahi kuchezea Shijaa msimu wa mwaka 2014-2015. Atasaidiwa majukumu ya unahodha na Michael Wanjala.

    Kocha mkuu wa timu hiyo Paul Murunga ametaja kikosi cha timu ya taifa ya raga huku akiongeza wachezaji wapya watano. Katika michuano ya Hamilton, Kenya imepangwa kundi moja na Afrika Kusini, Scotland na Ufaransa kwenye kundi C.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako