• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yasema iko tayari kufanya ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-01-18 09:56:46

    Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia amesema serikali yake iko tayari kushirikiana na nchi nyingine katika kanda yake katika mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa.

    Rais Farmajo amesema hayo jana alipozungumza na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa njia ya simu. Kundi la kigaidi la al-Shabab la Somalia tarehe 15 lilishambulia hoteli moja ya Kenya, na kusababisha vifo vya watu 21.

    Rais Farmajo amesema serikali ya Somalia siku zote inapenda kushirikiana na jirani zake ili kuzuia, kuondoa na kuushinda ugaidi.

    Kundi la al-Shabab limetangaza kufanya shambulizi hilo kujibu matamshi ya rais Donald Trump wa Marekani ya kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako