• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ni mwenzi asiyekosekana wa Afrika katika kutimiza "Ajenda ya Mwaka 2063"

    (GMT+08:00) 2019-01-18 10:39:15


    Mkutano wa 32 wa kilele wa Umoja wa Afrika utafanyika mwezi ujao mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mjumbe wa kudumu wa umoja huo nchini China Bw. Rahmat Mohamed Osman jana alipohojiwa na waandishi wetu wa habari alisema, China inatekeleza kihalisi ahadi yake ya kuiunga mkono Afrika kutimiza amani na maendeleo, na ni mwenzi asiyekosekana wa Afrika katika kutimiza "Ajenda ya Mwaka 2063".

    China inaendeleza uhusiano wa kiwenzi kati yake na Umoja wa Afrika kwa hatua madhubuti. Mwaka 2015, China ilianzisha tume yake katika Umoja wa Afrika, na mwaka jana ofisi ya umoja huo nchini China ilizinduliwa, ambapo Bw. Rahmat akawa mjumbe wa kwanza wa kudumu wa umoja huo nchini China. Bw. Rahmat anasema,

    " Kabla ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana mjini Beijing, pande hizo mbili zilishirikiana katika sekta mbalimbali. Sasa Umoja wa Afrika umepata kazi mpya ya kuratibu ushirikiano kati ya nchi za Afrika na China, na hii ni muhimu sana. Kuanzisha ofisi ya Umoja wa Afrika nchini China ni kwa ajili ya kuimarisha na kuhimiza uhusiano mzuri kati ya China na Afrika."

    "Ajenda ya Mwaka 2063" ni mpango wa malengo na hatua uliopitishwa mwaka 2015 na Umoja wa Afrika, na usalama na maendeleo ni malengo mawili muhimu. Bw. Rahmat anasema,

    "China haiingilii kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na msimamo huo unaungwa mkono na nchi za Afrika. Ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali umeinua uwezo wa Afrika, na kuisaidia Afrika kutimiza malengo ya maendeleo. Kati ya sekta hizo, amani na usalama ni muhimu zaidi kwa nchi zote za Afrika."

    Bw. Rahmat amesema ili kujenga Afrika mpya yenye amani, ustawi na umoja ndani ya miaka 50, Umoja wa Afrika unatakiwa kufanya mageuzi ya siasa na fedha, ili kutimiza maendeleo endelevu kwa kujitegemea na kujiamulia. Amesema uzoefu wa China ni mfano mzuri wa kuigwa. Anasema,

    "Uzoefu wa mageuzi ya China ni mfano mzuri wa kuigwa. Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, China imefanikiwa kuwasaidia watu milioni 700 vijijini kuondokana na umasikini. China imetupatia uzoefu wake katika maendeleo ya siasa, uchumi, maisha ya watu na viwanda, na kutunufaisha sana."

    Hivi sasa Bara la Afrika linaharakisha mchakato wa mafungamano na ujenzi wa eneo la biashara huria. Bw. Rahmat anaona kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linalingana na mahitaji ya nchi za Afrika katika kutimiza "Ajenda ya Mwaka 2063", na litaleta fursa nyingi za biashara na uwekezaji kwa Afrika. Anasema,

    " Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' linalingana na 'Ajenda ya Mwaka 2063'. Lengo letu la mwisho si miundombinu, bali ni kurahisisha mawasiliano kati ya nchi mbalimbali za Afrika. Naona kuwa tukiziunganisha tutapata mafanikio makubwa zaidi. Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' linahusiana na mambo mengi, ambayo yanahitajiwa na nchi za Afrika, na kuweza kuhimiza maendeleo yetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako