• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yapuuza madai ya Marekani juu ya uhamishaji wa teknolojia ya makombora kwa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2019-01-18 17:06:13

    Balozi wa Russia nchini Korea Kaskazini Alexander Matsegora amesema, madai ya Marekani kuwa Russia imeiuzia Korea Kaskazini teknolojia ya makombora na ulinzi wa anga ni ya kutungwa na hayana msingi wowote.

    Balozi Matsegora amesema Marekani pia inajaribu kuhalalisha sera zake zinazoyumba katika eneo la usalama wa kimataifa.

    Rais Donald Trump wa Mareklani jana alizindua Tathmini ya Ulinzi wa Makombora, ambayo inajumuisha dhamira ya nchi hiyo ya kuendeleza uwezo wake wa ulinzi wa makombora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako