• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ndogondogo nchini China zina fursa ya kupunguza kodi zao

    (GMT+08:00) 2019-01-18 17:11:10

    Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilitangaza sera mpya mfululizo ili kutia nguvu ya uhai sokoni, na kukabiliana na shinikizo la kupungua kwa ongezeko la uchumi. Sera iliyotangazwa kwanza ni kupunguza kodi za kampuni ndogondogo ili kuzinufaisha, ambayo itatekelezwa kwa miaka mitatu. Sera hiyo imechukuliwa kuwa mwanzo wa sera mfululizo zitakazotekelezwa na serikali ya China mwaka huu katika kupunguza kodi, na itahimiza maendeleo ya uchumi wa China.

    Serikali ya China imedokeza kuwa, sera ya kupunguza kodi na kuzinufaisha kampuni ndogondogo iliyoanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 mwezi Januari mwaka huu itanufaisha kampuni nyingi za China. Kampuni zenye thamani ya jumla ya mali chini ya yuan milioni 50, wafanyakazi chini ya 300, na mapato chini ya milioni 3, zitathibitishwa kuwa kampuni ndogondogo ambazo zitanufaika na sera hiyo. Kwa mujibu wa takwimu husika, zaidi ya asilimia 95 ya kampuni za China zimethibitishwa kuwa kampuni ndogondogo, asilimia 98 kati ya kampuni hizo ni kampuni binafsi.

    Licha ya kunufaisha idadi kubwa ya kampuni ndogondogo, kiasi cha kupunguza kodi pia ni kikubwa sana. Kampuni zenye mapato chini ya yuan milioni 100 zitalipa kodi ya asilimia 5, ambayo imepungua kwa asilimia 20 kuliko kodi ya kawaida, na kampuni zenye mapato kati ya yuan milioni 1 hadi 3 zitalipa kodi ya asilimia 10, ambayo imepungua kwa asilimia 15 kuliko kodi ya kawaida.

    Kutokana na kuwa uchumi wa dunia bado unakabiliwa na changamoto kubwa, na mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani bado haujatatuliwa, uchumi wa China bila shaka umeathirika, hasa kwenye sekta ya uchumi na biashara. Ikiwa kundi kubwa la pili la kiuchumi duniani, hatua itakazochukua China katika kukabiliana na wimbi linalopinga utandawazi duniani, si kama tu zitaamua mwelekeo wa maendeleo ya uchumi, bali pia zitaleta athari kubwa kwa ongezeko la uchumi wa dunia nzima.

    Kuanzia mwaka jana serikali ya China ilifanya uchunguzi kuhusu sera ya kupunguza kodi za kampuni ndogondogo kwa mara nne. Kutokana na takwimu za idara ya kodi nchini China, miezi 11 ya kwanza mwaka jana, thamani ya kupunguza kodi kwa mujibu wa sera nafuu za kodi imefikia yuan bilioni 184.

    Kutokana na hatua mpya za kupunguza kodi zilizotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilikadiria kuwa kodi zitakazolipa kampuni ndogondogo za China zitapungua kwa yuan bilioni 200 kila mwaka. Sera hiyo itatekelezwa kwa miaka mitatu, hivyo kwa jumla sera hiyo itazisaidia kampuni hizo kupunguza kodi yuan bilioni 600. Hatua hiyo bila shaka itaongeza uwezo wa uwekezaji na matumizi wa raia kwa muda mrefu, na kutia nguvu ya uhai sokoni.

    Maendeleo ya utulivu wa kampuni ndogondogo si kama tu zitatoa nafasi nyingi za ajira, bali pia zitasaidia utulivu wa jamii. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametambua kuwa, kampuni ndogondogo ni soko kuu la kutoa nafasi za ajira, kupunguza kodi zao ndiyo kuunga mkono nafasi za ajira. Aliona kuwa kuendeleza kampuni ndogondogo kunahusiana na utulivu wa maendeleo ya uchumi na utulivu wa nafasi za ajira.

    Kupunguza kodi hakika kutaathiri mapato ya kifedha ya serikali, hivyo waziri mkuu Bw Li Keqiang alizitaka serikali katika ngazi mbalimbali zipunguze matumizi ya kawaida.

    Mwaka jana wakati rais Xi Jinping wa China alipofanya mazungumzo na wakampuni binafsi, alisema kampuni binafsi na wakampuni binafsi ni sehemu muhimu, aliahidi kupunguza mzigo wa kampuni, kutatua tatizo la kukusanya fedha kwa kampuni binafsi, kuweka mazingira ya haki ya ushindani, kulinda usalama wa makampuni binafsi na mali zao, ili kuunga mkono maendeleo ya uvumbuzi ya kampuni binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako