• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TLTC yataka pembejeo za Tumbako zikipelwe kwa wakati

    (GMT+08:00) 2019-01-18 18:48:05

    Kampuni ya ununuzi wa tumbaki nchini Tanzania TLTC imesema zao la tumbako limepoteza ubora wake kutokana na kuchelewa kwa pembejeo kwa ajili ya zao hilo.

    Akizungumza na Radio China kimataifa, mkurugenzi wa sheria wa TLTC Richard Sinamtwa amesema kwa miaka mitatu mfululizo kumekuwa na ucheleweshaji wa pembejeo kwa wakulima na hivyo kuathiri ubora wa zao hilo.

    Ametaka pembejeo ziwe zinapelekwa kwa wakulima kwa wakati ili tumbaku inayozalishwa iwe na ubora unaotakiwa.

    Aidha Waziri wa Kilimo wa Tanzania Japhet Hasunga amesema kuwa kuanzia msimu ujao hatokubali kuona pembejeo zinacheleweshwa.

    Amesema pembejezo hazipaswi kuchelewa kwa kuwa msimu wa kilimo unajulikana kila mwaka, kwamba ikitokea zikachelewa atachukua hatua kwa uongozi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako