• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwanja cha ndege cha Ukunda chapigwa jeki

  (GMT+08:00) 2019-01-18 18:48:29

  Kiwanja cha ndege cha Ukanda nchini Kenya kimepigwa jeki baada ya Mamlaka ya safari za anga kutangaza ujenzi wa mnara wa kudhibiti safari za ndege kwa njia salama kwa gharama ya shilingi milioni 150.

  Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Gilbert Kibe amesema uwekezaji huo umetokana na kuongezeka kwa safari za ndege katika uwanja huo huku wengi wa wasafiri wakiwa watalii.

  Kibe amesema katika siku za hivi karibuni uwanja wa ndege wa Ukunda umeshuhudia msongamano mkubwa kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watalii lakini pindi mnara huo utakapojengwa hali hiyo itatibithiwa . Idadi ya watalii nchini Kenya imeongezeka kwa asilimia 31.2 mwaka jana. Tangu Disemba mwaka jana, uwanja wa Ukunda umeshuhudia safari za ndege 300.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako