• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter asifu umuhimu wa kujenga uhusiano wa kibalozi kwa China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-01-19 16:52:48

    Rais wa zamani wa Marekani Bw. Jimmy Carteramesema, tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 40 iliyopita, zimetoa mchango kwa ustawi wao amani na utulivu wa kikanda.

    Rais Carter amesema hayo kwenye kongamano la 7 la kituo cha Carter kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani. Amesema tangu zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1979, si kama tu uchumi wa nchi hizo mbili umeongezeka kwa kasi, bali pia kanda ya Asia Mashariki imeelekea kuwa na amani na utulivu, kutoka vita na migogoro ya zamani.

    Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesisitiza kuwa, suala la Taiwan ni suala kuu kwenye uhusiano kati ya China na Marekani. Sera ya kuwepo kwa China moja, na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, bado ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako