• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Ethiopia kufanya mashambulizi ya kujibu dhidi ya kundi la Al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2019-01-20 17:10:19

    Jeshi la Ethiopia limetangaza kuwa Ethiopia linajiandaa kufanya mashambulizi makubwa ya kujibu dhidi ya kundi la Al Shabaab, baada ya kundi hilo kushambulia msafara wa magari ya jeshi la Ethiopia karibu na mji wa Burhakaba wa Somalia.

    Taarifa ya jeshi la Ethiopia imesema wanajeshi wa Ethiopia waliweza kuzuia shambulizi hilo na kurudi kambini salama. Hata hivyo kundi la Al Shabaab limetangaza kuwa limewaua wanajeshi zaidi ya 50 wa Ethiopia.

    Ethiopia ina maelfu ya wanajeshi nchini Somalia ikiwa ni sehemu ya vikosi vya tume ya Umoja wa Afrika AMISOM, ambayo kazi yake ni kupambana na tishio la kundi la Al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako