• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China atoa salamu za pole kwa mwenzake wa Kenya kutokana na shambulizi la kigaidi

    (GMT+08:00) 2019-01-20 17:19:02

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ametoa salamu za pole kwa mwenzake wa Kenya Bibi Monica Juma, kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea mjini Nairobi.

    Bw. Wang Yi amesema China inalaani aina yoyote ya vitendo vya kigaidi, itaendelea kuiunga mkono Kenya kupambana na ugaidi, na juhudi zake za kulinda amani na utulivu.

    Habari nyingine zinasema Kenya imeimarisha usalama katika sehemu za umma ili kukabiliana na tishio la kigaidi. Kwa sasa ni vigumu kuingia kwenye majengo, ofisi na maduka, baada ya shambulizi la kigaidi lililotokea kwenye hoteli ya dusitD2.

    Polisi wa Kenya wamethibitisha kuwa watu 21 wameuawa na wengine wengi walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako