• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana mlipuko wa bomba la mafuta Mexico yafikia 79

    (GMT+08:00) 2019-01-21 08:17:40

    Waziri wa afya ya umma wa Mexico Bw. Jorge Alcocer amesema mlipuko wa bomba la mafuta uliotokea Ijumaa katikati ya jimbo la Hidalgo umesababisha vifo vya watu 79 na wengine 81 kujeruhiwa.

    Akiongea na wanahabari Bw. Alcocer amesema baadhi ya wahanga wamejeruhiwa vibaya baada ya kuungua zaidi ya asilimia 80 ya ngozi yao.

    Rais Andres Obrador wa Mexico aliyeingia madarakani Desemba mosi, amesema serikali yake itaendelea na hatua madhubuti za kupambana na wizi wa mafuta zilizoanza kutekelezwa tangu mwishoni mwa mwaka jana.

    Kwa mujibu wa takwimu mpya za serikali, wizi wa mafuta uliisababishia nchi hiyo hasara ya dola za kimarekani bilioni 3 mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako