• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim kufanyika Vietnam

    (GMT+08:00) 2019-01-21 09:19:41

    Shirika la habari la Bloomberg la Marekani limesema mkutano wa pili kati ya rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un unatarajiwa kufanyika nchini Vietnam.

    Shirika hilo limesema serikali ya Marekani imepanga kufanya mkutano huo huko Hanoi, Vietnam, lakini pia kuna uwezekano wa kufanyika kwenye mji wa pwani Da Nang au mji wa kusini Ho Chi Minh.

    Ikulu ya Marekani ijumaa iliyopita ilitangaza kuwa mkutano wa pili kati ya rais Trump na Bw. Kim Jong Un utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari, lakini haikudokeza utafanyika wapi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako