• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Manny Pacquiao amchakaza Mmarekani Adrien Broner, atuma salamu za vitisho kwa Mayweather

  (GMT+08:00) 2019-01-21 09:29:29

  Mwanamasumbwi, Manny Pacquiao kutoka Ufipino ameshinda pambano lake dhidi ya Mmarekani Adrien Broner kwa points na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBA Welterweight.

  Pambano hilo lilifanyika katika ukumbi wa MGM Grand Mjini Las Vegas, Marekani asubuhi ya kuamkia jana Jumapili. Majaji wote watatu wamempa Pacquiao pointi 117-111, 116-112, 116-112.

  Pacquiao (40) alimzidi Broner kwenye karibia raundi zote 12, jambo ambalo limefanya apate ushindi huo kiurahisi.

  Baada ya pambano hilo, Pacquiao alimtumia salamu Bondia mwenzake Floyd Mayweather kwa kumwambia kuwa akubali warudie pambano lingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako