• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA YA WANAWAKE: Ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara-JKT Queens yaishushia mvua ya magoli Yanga Princess

    (GMT+08:00) 2019-01-21 09:29:50

    Kikosi cha Yanga Princess jana kimekubali kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 8-1 dhidi ya JKT Queens kwenye mchezo wa ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League.

    JKT Queens wanafanikiwa kuwafunga watani wote wa jadi baada ya kuanza na Simba Uwanja wa Karume kwa kuifunga bao 1-0 na jana wameendeleza ubabe wao kwa Yanga Princess kwa ushindi wa mabao 8-1.

    Mechi nyingine Alliance Girls wameshinda bao 6-0 dhidi ya Evergreen Queens, Baobab Queens wameshinda mabao 3-1 dhidi ya Mapinduzi Queens.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako