• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GDP ya China ya mwaka jana yaongezeka kwa asilimia 6.6

    (GMT+08:00) 2019-01-21 17:37:41

    Mkuu wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Ning Jizhe amesema, takwimu za awali zinaonesha kuwa, mwaka jana pato la taifa GDP la China liliongezeka kwa asilimia 6.6 ikilinganishwa na mwaka 2017. Amesema mwaka huu China ina msingi, mazingira, imani na uwezo wa kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi.

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwaka jana kwa mara ya kwanza pato la taifa la China lilizidi yuan trilioni 9, sawa na dola trilioni 13.3 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.6 ikilinganishwa na mwaka 2017. Mkuu wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Ning Jizhe anasema,

    "Mwaka jana pato la taifa la China liliongezeka kwa asilimia 6.6. Kasi hii ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine nne zilizoko mbele zaidi duniani kwa ukubwa wa uchumi, na mchango wa China kwa ongezeko la uchumi wa dunia ni karibu asilimia 30."

    Mwaka jana mfumuko wa bei nchini China ulikuwa ni asilimia 2.1, ambayo ni chini kuliko asilimia 3 kama ilivyotarajiwa. Wakati huo huo ajira mijini zimeongezeka kwa milioni 13.6, na kiwango cha watu wasio na ajira mijini kimekuwa chini ya asilimia 5 kwa miezi kadhaa mfululizo. Aidha mwundo wa uchumi pia umeboreshwa. Bw. Ning anasema,

    "Mchango wa matumizi kwenye ongezeko la uchumi unafuatiliwa zaidi na watu. Na mwaka jana mchango huo ulikuwa asilimia 76.2, ambalo ni ongezeko la asilimia 18.6 ikilinganishwa na mwaka 2017. Mwundo wa uwekezaji pia umeboreshwa, na uwekezaji wa watu binafsi na uwekezaji kwa sekta ya uzalishaji umeongezeka kwa haraka. Aidha mwundo wa sekta za uchumi umeboreshwa, na sekta ya huduma imetoa mchango kama nguzo ya uchumi, na kuchukua asilimia 52.2 ya pato la taifa."

    Hivi karibuni baadhi ya mashirika ya kimataifa yameshusha makadirio yao kwa ongezeko la uchumi wa dunia. Kuhusu mustakbali wa maendeleo ya uchumi wa China, Bw. Ning amesema mabadiliko ya dunia na hali mpya ya China vimeleta fursa muhimu, kwa kuifanya China kushirikiana vizuri zaidi na nchi nyingine, ili kupata mafanikio ya pamoja. Amesema China ina soko kubwa la watu karibu bilioni 1.4, na uzoefu wa kuendeleza uchumi. Anasema,

    "Mwaka huu, uchumi wa China unakabiliwa zaidi na hali ya kutatanisha ya kimataifa pamoja na tatizo la ndani la mwundo wa uchumi. Lakini wakati tunapotambua matatizo na changamoto, pia tunapaswa kuona matumaini, fursa na mustakbali mzuri. Mwaka huu, China ina msingi, mazingira, imani na uwezo wa kudumisha mwelekeo mzuri wa uchumi, na kutimiza maendeleo mazuri na mfululizo ya uchumi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako